Ooh Masikini, by Jamhuri Jazz Band


x2

Ooh Masikini
Mimi nina balaa sana
Tabu ni nyingi
Zinazonikaabili miye
Nitafanya nini ooh
Ulimwengu
Niwe na maisha
Kama wenzangu

Nitafanya nini ooh
Ulimwengu
Niwe na maisha
Kama wenzangu



x2

Nitafanya nini ooh
Maisha yananiendea vibaya miye
Kila ninalofanya miye ooh
Mauti yangu yangojewa kwa raha miye
Hakuna wema duniani ooh
Iliyobaki tumuombe Manani

Nitafanya nini ooh
Maisha yananiendea vibaya miye
Kila ninalofanya miye ooh
Mauti yangu yangojewa kwa raha miye
Hakuna wema duniani ooh
Iliyobaki tumuombe Manani
Tuwe Salama

Ooh tuwe salama
Ooh tuwe salama



Wasiwasi Ondoa, by Jamhuri Jazz Band


x2

Ni nini Mama unalia ooo
Unalizwa nini ooo
Mimi ni wako wa zamani ooo
mwenzangu shaka ondoa

Ninapokuaga matata hayaishi nifanye nini sasa
Mwenzangu wanitafuta lawama mabaya mimi mwenzio



x4

Wasiwasi kwangu ondoa
jiepushe na majirani ooo
Mimi ni wako ooo

Wenzako wanaona wivu
Tunavyoishi mimi nawe
Mimi ni wako oo usife moyo



Mganga N°1, by Jamhuri Jazz Band


x3

walinitesa sana ndugu zangu,
na kweli walifanikiwa,
na furaha walipata vijana,
kusikia mimi sisemi



 

wanyama wabaya maana yake,
sio simba wala si tembo,
ni wanadamu wenye choyo,
iyooo yalaaa



 

kaniki nilivalishwa,
hata chale nilichanjwa,
na madawa nilipakwa,
iyoo yalaa



 

mgonjwa amezidiwa,
haya mwite mganga,
haya shika mkoba,
iyoo iyoo iyoo
iyoo iyoo iyoo

iyoo iyoo iyoo
iyoo iyoo iyoo



Simba Mwituni, by Jamhuri Jazz Band


x3

Aaee maria ee
Aaee maria ee
Bembeleza mwana oo
Msitu mkubwa oo
Safari ni ndefu tutaliwa na simba,
Oooo maria

Safari ni ndefu mama
Mwana analia ooo
Tutafanya nini ni mashaka sana
Oooo maria